Wachimbaji wadogo katika mgodi wa Musega kijiji cha Genkuru kata ya Nyarukoba wilayani Tarime
Mkoani Mara wakiponda mawe kwa ajili ya kuuzia wateja na badae kupembua na kupata dhahab
Zaidi ya vijana 250 wakiwemo wakina mama, na wazee
wamepata ajila katika mgodi wa wachimbaji wadogo wa Musega uliopo katika kijiji
cha Genkuru kata Nyarukoba Wilayani Tarime Mkoani Mara suala ambalo
limewasaidia kukidhi mahitaji yao huku baadhi ya vijana wakiondokana na uvamizi
wa migodi pamoja na uwindaji haramu ambao walikuwa wakifanya hapo awali kabla
ya kupata ajila hizokatika vijiji ambavyo ni jirani na hifadhi ya Mbuga ya
wanyama
Akiongea na
Gazeti hili mmoja wa wamiliki wa Mgodi huo Ngicho Daud alisema kuwa ameweza
kuajili vijana zaidi ya 250 wakiwemo wazee na akina mama.
“Kwa upande
wa vijana tumewaajili kwa lengo la kupunguza uvamizi wa migodi pamoja na uwindaji
haramu kwa sababu hapa wanafanya kazi masaa yote nakujipatia kipato
kikubwa”alisema Ngicho.
Aliongeza
kuwa mgodi huo ulianzishwa na watu
watatu lakini mpaka sasa watu wengi wameweza kujipatia ajila kupitia mgodi huo
japo anakumbwa na changamoto kama vile ukosefu wa vifaa vya kisasa, ,Maeneo ya
kutosha , Mtaji mkubwa kwa ajili ya kupanua Miradi ya uchimbaji huo.
Sibute Masero ni mmoja wa vija ambao wamepata
ajilia kupitia mgodi huo wa wachimbaji wadogo alisema kuwa ameamua kuacha suala
la uwindaji haramu na kujiingiza katika uchimbaji mdogo kwa lengo la kupata
kipato cha harari.
“Katika
uwindaji haramu niliweza kufungwa kilia gereza lakini nilifanikiwa kutoka
hivyo inabidi niendelee na kazi yangu ya
uchimbaji mdogo ili kupata kipato changu” alisema Sibute.
Kwa upande
wake Pusinya Kichugu mkazi wa Kijiji cha Genkuru alisema kuwa kutokana na
kununua mawe hayo ameweza kusomesha watoto wawili sekondari na kukidhi mahitaji
yake yote ya Nyumbani.
Wakina mama
tuliowengi tunategemea Machimbo haya madogo kikubwa tunaomba serikali
iltuletee vifaa vya kisasa ili tuweze
kuboresha uchimbaji wetu alisema Pusinya
….MWISHO…
No comments:
Post a Comment