picha ya kapten wa Timu ya mafundi fc akikabidhiwa kikombe na OCD wa Tarime Issa Bukuku kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya Lazaro Mambosasa
Isticama walzawa kichapo cha bao 1-0
dhidi ya Mafundi fc:
Timu ya
Isticama Fc imelazwa kichapo cha bao 1-0 katika fainali za michuano ya
kembaki Cup zilizokuwa zikiendelea walayani hapa katika uwanja wa shamba la
Bibi Serengeti.
Katika
mashindano hayo zilizweza mushiriki timu kumi na mbili kwa njia ya mutoano
ndipo zilibakia timu sita na kuwa na makundi ya A na B ambapo zilitoka timu
mbili Mafundi Fc na Isticama nakuingia fainali.
Katika
michuano hiyo timu zote mbili ziliweza kuoneshana ubabe na ndipo dk ya 80
kipindi cha pili mafundi Fc walichungulia nyavu za Isticama kupitia kwa Ibraim
sabiro bao ambalo li;lidumu mpaka dk 90
za mchezo huo zinaisha.
Katika
michuano hiyo ya Kembaki Cup2013-2014 mshindi wa kwanza ambaye ni Mafundi Fc
walijinyakulia kombe na shilingi laki Tano, Mshindi wa pili laki Tatu ambaye ni
Isticama Fc huku mshindi wa pili Kenyamanyori Fc laki mbili.
Michael
Kembaki ambaye ni mdhamini wa michezo
alisema kuwa lengo la michezo hiyo ni kuwezesha vijana kujituma katika utendaji
wa kazi kupitia michezo.
“Michezo ni
burudani kupitia michezo hii vijana watajituma hivyo tutazidi kuboresha michezo
kwani hii ni awamu ya pili nikidhamini michezo na mwakani nitaongeza zawadi”
alisema Kembaki.
Kwa upande wake katibu wa chama cha mpira
wilayani Tarime(TAFA) Brandani Mtatiro
aliwataka viongozi wa virabu kutumia kanuni 17 za michezo ili kuboresha michezo.
“Viongozi wa
virabu wasipotumia kanuni zote za mpira bado changamoto zitzidi kujitokeza”
alisema katibu wa chama cha mpira.
Naye OCD Wa wilaya Issa Bukuku kwa niaba ya
kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Tarime Rorya aliwataka vijana kupenda
michezo huku wakizidi kudumisha Amani
“Michezo
bila amani haiwezekani hivyo tuendelee kudumishsha Amani ili kuboresha Michezo”
alisema.
…..Mwisho…
No comments:
Post a Comment