MAHAKAMA ya Mwanzo
Ryagoro Wilayani Rorya Mkoani Mara imechomwa Moto na watu wasiofahamika na
kuteketeza chumba cha masijala pamona na vielelezo vya kumbukumbu za mafaili
kuteketea.
Akisimulia tukio hilo
kwa waandishi wa habari Kamanda Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya kamishina
msaidizi wa Jeshi la polisi ACP Lazaro Mambosasa alisema kuwa tukio hilo
lilitokea saa 3.30 usiku kuamkia November 09 mwaka huu.
''Jengo la Mahakama ya
Mwanzo Ryagoro lilichomwa moto na watu wasiojulikana chumba kilichoathirika
zaidi ni chumba cha masijala ya mahakama hiyo dhamani ya mali iliyoungulia
ndani ikiwa ni majalada pamoja na samani nyingine ni Tsh 5,000,000''alisema
Mambosasa.
Aidha Mambosasa
aliongeza kuwa hakuna Mtu yeyote ambaye anashikiliwa kuhusiana nan tukio hilo
na kuwa chanzo cha tukio bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea
kufanya upelelezi kuwapata watuhumiwa wa tukio hilo na kuwafikisha kunako
husika.
Kwa upande wa wananchi
wa kutoka eneo la tukio walisema kuwa mahakama hiyo iliunguzwa saa 2 usiku
kuamkia Novemba,9 mwaka huu na watu ambao wanasadikiwa kuwa ni watuhumiwa wa
makosa mbalimbali.
''Vijana walikuwa
wanatoka usiku katika majumba ya kuonyesha mpira gafula walipita wakaona
Jengo la mahakama linaungua moto ambapo walipiga mwana ili kuomba msaada ambapo
wananchi walifika na kutoa msaada wa kuokoa mali zilizokuwemo ndani
yake''walisema wananchi hao.
Aidha wananchi hao ambao
hawakutaka majina yao yatajwe Gazetini walisema kuwa kuchomwa moto mahakama
hiyo ni kupoteza kumbukumbu za mafaili ya watuhumiwa ambao walikuwa
wanashitakiwa mahakamani hapo.
''Tunaomba serikali
ichukue hatua za haraka kuwasaka watuhumiwa wa tuykio hilo kwa sababu kitendo
hiki hakifurahishi jamii na kina lengo la kudididmiza wanyonge''walisema
wananchi hao.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment