Sunday, November 9, 2014

Vijana watakiwa kulinda nguvu ya Taifa



Naibu mwenyekiti wa baraza la wanawake BAWACHA Hawa mwaifunga akiongea na wananchi kwenye mkutano wa adhara kuhusu rasimu ya katiba

Vijana wametakiwa kulinda nguvu ya Taifa ikiwa ni pamoja na kufanya mapinduzi na maamuzi ya kweli ili kuweza kupata viongozi na si kuchagua viongozi mizigo ambao watachosha wananchi na kufuja mali za umma 

Kauli hiyo Mratibu wa uhamasishaji wa vijana Chadema Taifa Edward Simbey  katika mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni katika mji mdogo wa Utegi  wilayani Rorya Mkoani Mara katika mwendelezo wa ziara ya kuelimisha wananchi kuhusu chaguzi za serikali za mitaa pamoja na maoni juu rasmu ya katiba mpya  huku wakiambatana na viogozi wa kitaifa Balaza la akina Mamakupitia Chama Cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA chini ya Mwenyekiti akina Mama Bawacha Taifa Halima Mdee.

 Edward alisema kuwa taifa lolote duniani vijana ndo nguvu kazi ya taifa katika chachu ya kusukuma gurudumu la Maendeleo ikiwemo na wilaya ya Rorya.

Aidha  Mratibu wa vijana aliwataka vijana hao Vijana waoneshe nguvu ya jeshi ili kuwepo upambanaji wa kweli mpaka haki inapatikana huku akilaani jeshila polisi kuondokana na kunyanyasa vijana na kuwageuza mitaji na kuwatengenezea kesi zisizokuwa za msingi ili kuweza kujipatia maslahi.

Kwa upande wakeMbunge wa Viti maalumu Ester Matiko ambaye pia ni Mwenyekiti akina Mama Mkoa wa Mara  alisema kuwa akina mama hospitalini wamezidi kuangaika na kununua madawa wakati serikali inazidi kutumia fedha kubwa katika mambo yasiyo ya msingi.

“Wanafunzi sasa wanatahabika kwa kukosa  Madawati, Madarasa yanadodondoka kwanini nhizo fedha serikali inazoharibu zisije kujenga shule na kununua madawati” alisema.

 Naye katibu wa Mkoa mkoa wa Mara Chacha Heche amezidi kulaani viongozi wanaotumia ubabe kunyanyasa wananchi kuondoka na  vitendo hivyo mara moja.

Hata hivyo meya wa manispaa ya musoma Alex Kisurula  alisema kuwa alisema kuwa maendeleo yanletwa na viongozi wenye uzalendo pamoja na siyo viongozi wanaojitapa kwa utajili walionao wakati wananchi wanazidi kutaabika.

Maisha yangu yanfanana na wananchi wa ngu lakini nyie wananchi wa Rorya maisha mbunge wenu yanafanana na ya kwenu alisema meya.

Pia meya huyo aliwataka wananchi wa rorya kuondokana na vijazawadi wanavyopatiwa  na kubadilisha mawazo katika kupiga kura na kuchagua viongozi wabovu. 
                                                 ....mwisho.........

No comments:

Post a Comment