Wednesday, November 12, 2014

WATOTO NJITI (PRE-TERM BABIES)



    
Watoto njiti ni(Pre-term babies) wale watoto wote wanaozaliwa kabla ya kutimiza wiki 37 tangu tarehe ya kwanza ya mama kuona hedhi yake ya mwisho,bila kujali uzito aliozaliwa nao mtoto huyo. Kwa kawaida mtoto  anaweza kuishi vizuri nje ya mfuko wa uzazi pale anapotimiza  wiki 37 na kuendelea. Mtoto anaweza kuzaliwa muda wowote kuanzia wiki ya 37-42. Baada ya wiki ya 42 kumalizika mama akiwa hajajifungua basi hiyo mimba tunasema imepitiliza muda ( post-term pregnancy) na juhudi  za kumzalisha mama huyu huanza mara moja.

Hapa lazima kutofautisha na wale watoto wanaozaliwa wakiwa na uzito chini ya wastani ambao huwa wametimiza  wiki 37 ama zaidi(low birth weight /small for gestation age).  Kwa kawida mtoto anatakiwa wakati wa kuzaliwa awe na uzito  wa 2.5kg-4.5kg.

          SABABU ZA KUZAA MTOTO NJITI
Sababu za za kuzaa mtoto njiti zimegawanyika katika makundi yafuatayo:-

(A)- Zile zitokanazo na mtoto( Fetal Causes)
i/ mtoto kupata shida ya kupumua kutokana na kiasi cha hewa ya oksijeni kupungua katika mzunguko wa damu wa mama ama mtoto( fetal distress).

ii/Watoto mapacha( twins pregnancy) ,ambao  huwa uzito mkubwa kuliko mtoto mmoja, uzito huo hukandamiza mlango wa kizazi (cervix) hivyo kusababisha  mlango wa kizazi kufunguka kbla ya wiki 37

iii/ kuwa na  chembe nyekundu za damu zisizo fanya kazi katika mzunguko wa damu wa mtoto(Erythroblasis), chembe nyekundu za damu zinahusika kusafirisha hewa mwilini . upungufu wa chembe chembe nyekundu  hizo husababisha mtoto kupata shida ya upumuaji.

(b)Plasenta( placental causes)
i/ plasenta kutofanya kazi vizuri (placental disfunction).plasenta ni kiungo kinachoounganisha mtoto na mama , hutumika kupitisha mahitaji toka kwa mama ;mfano virutubisho, hewa ya oksijeni nk . pia kutoka kwa mtoto kwenda kwa mama kama vile taka mwili mfano hewa ya ukaa( carbondioxide). Placenta isipofanya kazi vizuri inaathiri kazi hizo hivyo mtoto anaweza kuzaliwa kabla ya muda kutimia ama mimba kutoka.

ii/placenta kujishikiza katk sehemu ya chini karibu na mlango wa kizazi(placental praevia).placenta kwa kawaida inajishikiza sehemu ya juu ya mji wa mimba( fundus of the uterus) ambayo ina misuli iliyo imara zaidi kuweza kuhimili uzito wa mtoto. Sehemu ya chini haina misuli ya kutosha kuhimili uzito hivyo  placenta kuachia na mimba kutoka ama kuzaliwa mtoto njiti.

iii/placenta kujiachia mapema  kutoka katika ukuta wa kizazi kabla ya  wiki 37 ya umri wa mimba kutimia’ kutoka katika sehemu ya kawida ilipojishikiza.(placental abruption) hivyo kusababisha mtoto kuzaliwa  kabla ya muda kutimia. Pia sababu hii inaweza kupelekea mama kupoteza damu damu nyingi kabla, wakati na baada ya kujifungua.

(c)mji  wa mimba(uterine causes)

i/Biconuate uterus mfuko wa uzazi kuwa na umbo lisilo la kawaida hivyo kutoshikilia mtoto vizuri
ii/mlangp wa kizazi kutokuwa imara hivyo kufunguka mapema kabla ya mimba kufikisha wiki 37( incompetent cervix), ambapo huzidiwa na uzito wa mtoto, akina mama wenye tatizo hilo hukumbwa na tatizo la mimba tatu au zaid kutoka bila sababu yoyote ya msingi kati ya wiki  ya................
Tatizo hilo hutibiwa kwa kufunga shingo ya kizazi  kwa nyuzi maalumu kati ya wiki ya 13-16 kitalaamu inaitwa cervical cerclage .mama atafunguliwa nyuzi hizo  mimba inapotimiza wiki 37 ama muda mfupi kabla ya uchungu kuanza.
(d)sababu zinazomhusu mama(maternal causes)
i/mama kuwa na maji mengi katika chupa ya uzazi(polyhydromnious). Mama hupimwa kiasi cha maji (amniotic fluid index), ili kujua kama maji ni kidogo(oligohydromnious, maji ni ya kawaida(adequate amniotic fluid, ama ni mengi(polyhydrominous) maji katika mfuko wa uzazi yanamkinga mtoto kujigonga vilevile kusaidia mtoto kukaa vizuri yaani supporting. Maji yanapokuwa mengi yanazidisha uzito,hivyo kuongeza mkandamizo katika mlango wa uzazi, hivyo kuwahi kufunguka.dalili ya maji kuwa mengi katika mfuko wa uzazi ni mama kuwa na tumbo kubwa kuliko umri wa mimba( hingh fundal height for gestation age) pia mama anaweza wakati mwingine kulalamika vichomi
ii/ mama kupata kupata tatizo litokanalo na  kutumia dawa wakati wa matibabu.inaweza kuwa kwa kuzidisha kiwago kinachotakiwa(drug overdose) ama kutumia dawa ambayo hairuhusiwa wakati ama wote au kupindi Fulani cha ujauzito(drug contraindications in pregnancy)Madawa yanakazi maalumu( drug indications) pia kuna madawa hayaruhusiwa katika hali Fulani kama ujauzito, kumbe dawa hiyo ikitumika inaweza kusababisha mimba kutoka ama kuzaliwa mtoto mwenye matatizo ya kimaumbile ama kuzaliwa mtoto kabla ya muda kutimia yaani mtoto njiti. Mfano ALU katika miezi mitatu ya kwanza, misoprostol wakati wote wa ujauzito na mengineyo
iii/kifafa cha mimba(pre-enclampsia)
iv/magonjwa sugu( chronic diseases) kama vile kisukari
v/ utumiaji wa pombe kali na/ madawa kulevya kama vile kokaini

(e)sababu nyinginezo
i/Chupa ya maji kupasuka kabla ya wiki 37(pre –term premature rupture of membrane,pprom)
ii/sababu nyingine ni kama ajali,kupigwa nk
iii/magonjwa ambukizi pia magonjwa sugu

               JINSI YA KUMTAMBUA MTOTO NJITI
i/kuangalia tarehe ya kwanza mama alipoziona siku zake za mwisho wanaita kutumika ,kama muda huo ni chini ya wiki 37 bas mtoto huyo atakuwa njiti(pre –term baby). Hata hivyo njia hii haitumiki saana kutokana na sababu kuwa akinamama wengi hawakumbuki kwa usahihi tarehe ya siku ya kwanza kuona hedhi yake  ya mwisho(wrong date),
ii/ngozi ya mtoto njiti inakuwa kama inanata mfaano wa ngozi iliyopakwa mafuta mazito kama vile grisi ama kimiminika kama asali
ii/chuchu Breast nodule za mtoto njiti hazionekani vizuri wakati za mtoto aliyetimiza muda chuchu zinaonekana vizuri
iii/mtoto njiti hana mistari inayopatikana viganjani na miguuni(Sole creases)
iv/mtoto njiti ana nywele kidogo ukiliinganisha na zile mtoto aliyetimiza muda anazokuwa nazo
v/sehemu za siri za mtoto njiti mfano mfuko wa korodani hauna mikunjo na pia ile sehemu ya nje ya uke wa mtoto wa kike zinatofautiana zaidi.

NB: Mama apelekwe sehemu yenye uwezo wa kutoa huduma ya afya yenye vifaa na wataalamu ili kupata huduma stahili(in utero-transfer). Ikiwemo jitihada za kuzuia mama kujifungua,ama kupewa dawa ya kukomeza mapafu ya mtoto inayofanya kazi masaa ishirini na nne kabla ya mama kujifungua mtoto njiti kukomaza mapafu kwa kuongeza kimiminika kinachosaidia mapafu kutanuka na kusinyaa kwa urahisi wakati wa upumuaji(surfactant) kwa kuchomwa sindano ya dawa inayojulikana kitalaamu kama………………….

               MAMBO YA KUZINGATIA KWA MTOTO NJITI
Mtoto anapozaliwa njiti mwili wake unakuwa haujakamilika kuweza kujitegemea nje ya mama. Hivyo mtoto huyo anaweza kupata matatizo yafuatayo ambayo yanaweza kupelekea mtoto kupoteza maisha .

(a)joto la mwili kupungua(hypothermia) mtoto mdogo huwa anapoteza joto kwa haraka zaidi hivyo lazima kuhakikisha anatunzwa vizuri kwa kutumia njia kama vile kumfunika nguo,kumweka katika mashine maalum(incubators), kumweka  kifuani kwa mama (kangaroo mother caring, pia kuepuka kumwogesha mtoto mpaka ile siu aliyotarajiwa kuzaliwa ifike. Delay bath till expected day of birth
(b)kiasi cha sukari kushuka(hypoglycaemia).kiwango cha sukari katka damu ya mtoto kipimwe, pia mtoto alishwe vizuri kwa kutumia kanuni za kitalaamu( neonatal feeding formula)
(c)Kupata ugumu wa kupumua(fetal distress syndrome) Hii ni kwa sababu mapafu ya mtoto yanakuwa hayajakomaa kumwezesha kupumua vizuri
(d)homa kali itokanayo na wadudu kutokana na kutozingatia usafi kwa mtoto( Neonatal sepsis) Mtoto asipewe chanjo mpaka pale uzito wake unapotimia kilo mbili ama zaidi
(e)Magonjwa ya kuvuja damu( haemorrhagic diseases)  mtoto anatakiwa achomwe vitamin K ili kusaidia kupunguza tatizo hilo kwa kusaidia damu kuganda.
(f) kama mtoto amezaliwa akashindwa / ama akachelewa kulia basi inabidi asadiwe kupumua kwa vifaa maalumu (resuscitation)
(g)kuzuia mtoto asipoteze maji mwilini kwa kumtathimini kiasi cha maji(hydration status)

          DALILI ZA HATARI KWA MTOTO NJITI
Dalili zifuatazo ni za hatari kwa mtoto njiti na zinahitaji kuchukua hatua mara moja. Kama mtoto yuko kwenye hospitali ambayo haina vifaa na wataalam basi mtoto apelekwe mara moja kwenye huduma stahiki
i/joto la mwili kushuka(hypothermia) ama joto la mwili kupanda(hyperthermia)
II/Tumbo kujaaa(distended abdomen)
Iii/mtoto kuvuja damu( bleeding) na kuwa na njano katika viganja vya mikono na miguu(neonatal  jaundice)
IV/mapigo ya moyo  kuwa chini ama juu kuliko ilivyo kawaida,msukumo wa damu (blood pressure) kuwa chini(high blood pressure)/juu(high blood pressure) kuliko kawaida
v/mtoto kulegea/ ama kukataa/kushindwa kula(, Lethargy& refusal to feed)
vi/mtoto kutetema(Seizures)

JINSI YA KUTUNZA WATOTO NJITI  KATIKA CHUMBA MAALUM
Watoto njiti wako katika hatari kubwa ya kupoteza maisha kutokana na joto la mwili kushuka chini ya wastani, (hypothermia). Sababu zikiwa ni kuwa na ziada ndogo ya nishati(less energy store), kuwa na kiasi kidogo cha mafuta chini ya ngozi yanayozuia joto kupotea(, less insulating fat), mfumo hafifu wa kurekebisha joto mwili(poor heat regulating mechanism), kasi kubwa ya kupoteza joto kwa sababu ya umbo dogo (large surface area to volume ratio).
Tathimini hufanyika ili kujua mtoto njiti yupi anahitaji kuwekwa katika mashine maaluum ya joto kitaalamu inajulikana kama incubator. Watoto njiti wanaweza kuwa wale waliozaliwa kabla ya wiki 28 kutimia, wale wanaozaliwa kati ya wiki ya 28-32  ama wale wanaozaliwa kati ya wiki 32-37.
Pia uzito wa mtoto wakati wa kuzaliwa ni muhimu sana kwani husaidia kujua wastani wa joto ambalo mtoto anahitaji ili mifumo yake ya mwili iweze kufanya kazi vizuri. Jedwali lifuatalo linaonyesha
uzito wa mtoto na kiasi cha joto la mashine linalohitajika ili kumwezesha mtoto huyo kuishi
.
Uzito wa mtoto(Kg)
   Joto la chumba/ mashine (0C)


1.0 – 1.5
34 – 35


1.5 – 2.0
32 – 34


2.0 – 2.5
30 – 32


> 2.5
28 - 30














Zifuatazo ni njia zinazotumika ili kuhakikisha kuwa mtoto anawekwa katika mazingira ambayo yatamwezesha  kuishi vizuri.
i/ Kuhakikisha  ngozi ya mtoto inakuwa imegusana na ngozi ya mama ( skin to  skin contact/ kangaroo mother care). Hapa mama anashauriwa kumbeba mtoto kwa kumgusisha katk ngozi ya mama uda mwingi ili kumkinga mtoto kupoteza joto.
15

Ii/Kumfunika mtoto kwa nguo nzito iliasipoteze joto. Nguo hizo lazima ziwe safi muda wote ili mtoto asipate homa itokanayo na vijidudu kama vile bacteria nk (sepsis)
Untitled-8
IMG_0337
4

ii/ Njia nyingine ni kuwaweka watoto hao katika mashine maalum yenye hewa iliyopashwa joto(Air-heated Incubator) ambayo ina joto kadri ya mahitaji ya mtoto njiti.

Untitled-7

iii/ Njia nyingine ni kutumia matandiko  ambayo yana mzunguko wa maji yaliyopashwa joto(Heated water-filled mattress)

 Untitled-7

Iv/Mashine nyingine ni ile inayotoa joto ambalo humfikia mtoto  mfano wa joto la jua linavyotufikia(Overhead Radiant warmer).Ambayo picha yake imeonyeshwa hapa chini. Mashine hizi zote zinahitaji uangalizi wa karibu sana muda wote mtoto awekwapo katika mashine hizo ili kkugundua mabadiliko yoyote kwa mtoto na kuchukua hatua mara moja

IMG_0334
Overhead Radiant warmer

v/ Njia nyingine ni kumpaka mtoto mafuta(Oil application) mafuta husaidia kuziba vitundu vidogovidogo vilivyo katika vinyweleo katika ngozi ya mwili ili kuzuia joto kupttea kupitia vitundu hivyo
infant

Vi/ Njia nyingine ni kumfunika mtoto kwa mfuko maalum unaojulikana kama polythene sheet.mfuko huu ni maalumu kwa watoto lakini unafanya kazi sawa na mifuko mingine wanayotumia mama ntilie kufunikia vyakula visipoe kama vile maandazi na wali,kwa sababu unazuia joto kupotea
7211289f1

Vi/ mtoto azaliwapo mwili wake huwa umefunikwa na kitu  mafuta mazito kama girisi,( Vernix caseosa) wengine huona kama ni uchafu la! Kama mtoto amezaliwa njiti usijaribu kutoa maana utasababisha ngozi ya  mtoto kuwa wazi hivyo kupoteza joto kwa wingi.

Vii/ Mtoto njiti asiogeshwe mpaka siku aliyo tarajiwa kuzaliwa ifike, hivyo hakikisha mazingira ya kumhudumia yanazingatia usafi wa hali ya juu(Neonatal Intensive Care Unit Protocol)
VIII/ Hakikisha mtoto anapata lishe kwa mujibu wa taratibu za kulisha watoto njiti(Neonatal and low birth weight feeding schedule
IMG_0331
                            Gavage feeding





IMG_0330
Spoon feeding


No comments:

Post a Comment