Ligi ya Mbunge wa viti maalumu jimbo la Tarime kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ester Matiko imetoa hamasa kubwa vijijini kwani vijana wengi wataweza kushiriki ligi hiyo na kuendeleza kukuza vipaji.
Mratibu wa
mashindano hayo Martin Kebacho kipindi akigawa mipira katika kata 30 zilizopo ndani ya Wilaya na
Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa ajili ya mazoezi ili kujiandaa na michuano
ambayo itaanza 20 Novemba katika viwanja tofauti kwa kuhusisha timu
zilizoandaliwa kutokana na kata hiska.
Vijana
walisema kuwa michuano hiyo imekuja tofauti kwani michuano mingine vijana wa vijijini wamekuwa wakisikia maeneo
ya mijini tu na maeneo mengine hivyo suala hilo limewapa hamasa kubwa.
“Mashindano
kama haya tumekuwa tukiyasikia maeneo ya mjini sasa tunajivunia kushiriki
mashindano ya mbunge wetu” walisema vijana.
Mratibu wa
michezo aliongeza kuwa zitashiriki kata zote 30 na timu zitacheza kata kwa kata
na kuweza kupata timu 16 pia zitarudiana mara ya pili na kupata tena timu 8
ambapo timu hizo zitaanza ligi mojo kwa moja ili kuweza kupata mshindi wa
kwanza mpaka wa tatu.
Aidha
aliongeza kuewa kwa timu nane zitakazobahatika kuingia nane bora kwanza
zitapata jenzi seti moja moja pia mshindi wa kwanza atapewa zawdi ya kombe na
laki saba wapili laki tano na watatu laki tatu
Kwa upande
wake mdhamini wa michuano hiyo Ester Matiko alisema kuwa lengo la michuanoi
hiyo ni kukutanisha vijana wote kupitia vijiji, vitongoji na kata ili waweze
kubadilishana mawazo.
“Kuhusu
akina mama sijawasahau nitaweza kuanzisha michezo minginembalimbali ambayo
wanaweza kushiriki kwani nimesimama kwenye kiti cha uongozi kwa sababu ya akina
mama”alisema Ester.
…..Mwisho…
No comments:
Post a Comment