Thursday, November 6, 2014

WAOMBOLEZAJI WASHUSHIWA KIPIGO NA POLISI- TARIME


Katika hali isiyokuwa  ya kawaida waombolezaji wa mazishi ya kijana John msonso Christopher wa kijiji cha Kewanja wilayabi Tarime  mkoani Mara alie uawa kwa kuvunjwa shingo na watu wasio julikana, wamepata kipigo kutoka kwa askari  polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya na kusababisha watu watatu kulazwa katika kituo cha afya cha nyangoto wilayani humo  


 Bw Mahanga buruna nahanga mkazi wa kijiji cha kewancha kitongoji cha magena ni mmoja kati ya watu walio jeruhiwa.

Kutoka na tukio hilo katibu wa ccm wa wilaya ya Tarime Bw Bogomba Rashidi na mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha kewanja  Bw Tanzania Omtima ambao ni baadhi ya mashuhuda na ni  kati ya waombolezaji walio nusurika kupata kipigo kutoka kwa askari hao wamewataka vijana hasa wanao ishi kata ya matongo na kemambao kutii sharia bila shuruti ili kupunguza migogoro inayo jitokeza mara kwa mara baina ya polisi na vijana wa  kata hizo

 migogoro hiyo inasababisha baadhi ya vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kupoteza maisha uku takwimu zikionyesha kwamba kila mwezi vijana watatu mpaka watano wa vijiji vinavyo zunguka mgodi huo hupoteza maisha na kuacha wajane na watoto yatima  ambao badae watakuwa mzigo mkubwa kwa serikali katika kuwatunza

Pia viongozi hao wamelitaka jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya nalo lisitumie nguvu nyingi kupita kiasi katika kupambana na wananchi wa kata hizo na badara yake wawakamate watuhumiwa na kuwafikisha katika vyombo vya sharia  

                                                        Mwisho

No comments:

Post a Comment