Wednesday, November 5, 2014

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime azidi kuungamkono wananchi katika ujenzi wa maabara.






Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambaye pia ni diwani wa kata ya Sirari amezidi kuonesha moyo wa kuchangia ujenzi wa maabara unaoendelea katika shule za sekondari wilayani Tarime ili kuweza kuwaunga mkono wananchi.

Mwenyekiti huyo ikiwa ni moja ya kukagua miradi ya ujenzi wa maabara hizo ameweza kutoa msaada wa mifuko 13 ya saruji katika shule ya sekondari Kibasuka ambapo hivi karibuni ameweza kutoa mifuko 10 ya sarujiu katika shule ya sekondari Mwema kwa lengo la kuwaunga  mkono wananchi hao.

Sagara alisema kuwa suala la ujenzi wa maabara ni la kila mtu hivyo wananchi hao hawana budi kuzidi kuonesha mshikamano, Umoja na Nguvu ili kuweza kukamilisha ujenzi huo.

“Sisi kama serikali wale ambao wataonesha moyo wa kujenga tutawapa kipaumbele pale tutakapo anza kusambaza fedha za kusaidia kusukuma ujenzi huo” alisema sagara.
Kwa upande wake Mtendaji wa kata ya Kibasuka Mwita Marwa Mtatiro alisema kuwa yeye ameweza kutumia njia ya kuamasisha kupitia rika(Saiga) suala ambalo limeweza kusaidia katika kusukuma ujenzi huo kwa kiasi kikubwa sana.

“Jengo moja tayari limefikia katika renta hii yote ni nguvu ya wananchi na hapa wamekusanyika wanazidi kujadili na kurejesha michango”alisema Mtendaji.

Naye Diwani wa kata hiyo Joseph Moya Suleiman alizidi kuwataka wadau wote wa maendeleo wakiwemo wafanyabihashara kuzidi kujitolea kwa lengo la  kufanikisha

“Maabara ni kwa ajili ya watoto wetu endapo tutamaliza ujenzi huu tutazalisha wanasayansi wengi kutokana na shule zetu za kata” alisema Moya.

                                              …..MWISHO…

No comments:

Post a Comment