Chama cha
mapinduzi wilayani Rorya Mkoani mara kimezindua shina la Umoja wa Vijana Chama
Cha Mapinduzi (UVCCM) Boda boda katika stendi
ya Utegi wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuchomwa kwa kadi zaidi ya miamoja
za umoja wa katiba ya wananchi
(UKAWA)zilizorejeshwa na baadhi ya wanachama wa
vyama vya tofauti tofauti vya upinzani.
Akifungua
shina hilo la waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda Mbunge wa jimbo la Rorya
Lameck Aairo aliwataka vijana hao kuzidi kudumisha umoja wao ikiwa ni pamoja na kuondokana na
suala la kutumiwa vibaya na wanasiasa kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Aaidha
Mbunge huyo amesema kuwa ahadi ambayo alihaidi hapo awali itatimizwa mnamo Desemba
mwaka huu ili kuwapa hamasa waendesha pikipiki hao.
“Pikipiki
mbili ambazo niliahaidi kwa sasa ziko bandarini kufiki mwezi Desemba zitakuwa
zimefika na nitaweza kuwakabidhi rasmi” alisema Mbunge.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Rorya Samwel Kibo(Maarufu
kama namba tatu) aliwataka waendesha boda boda hao kufungua akaunti ili kuweza
kutunza fedha zao katika hali ya usalama.
Aaidha
Mwenyekiti huyo aliweza kutoa laki moja
kwa lengo la kuwawezesha vijana hao kufungua akaunti hiyo huku akihaidi baada
ya kufunguliwa atawapatia shilingi million mbili.
“Fungueni
maramoja akaunti alafu niletee taarifa nitawapa millioni mbili kwa lengo la
kutunisha mfuko wenu” alisema Mwenyekiti.
Jerard
Bitaris ni moja wa waendesha pikipiki
maarufu kama bodaboda alisema kuwa viongozi hawana budi kuwasaidia katika
kutatua changamoto zinazowakabiri ili waweze kujikwamua kiuchumi.
“Tunakumbwa
na changamoto nyingi katika utendaji kazi wetu hivyo viongozi wazidi kutusaidia
ili tuweze kujikwamua kiuchumi kwani waliwengi tunatumia pikipiki zisizokuwa
zetu” alisema Jerard.
……Mwisho…
No comments:
Post a Comment