Wednesday, November 19, 2014

CHADEMA WAKEMEA MANYANYASO.


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara kimelaani vitendo wanavyofanyiwa baadhi ya viongozi wa chama hicho ikiwa ni kukamatwa pasipo sababu za msingi na kuwekwa ndani pasipokuwa na dhamana yeyote huku wakibambikiziwa kesi mbalimbali.
 
Kauli hiyo imetolewa  na baadhi ya viongozi wa chama hicho katika kikao ilichofanyika kwenye ofisi ya (CHADEMA) Manispaa ya Musoma ili kuweza kuangalia mstakabali wa uchaguzi wa serikali za mitaa zijazo hapo mbeleni.

Chacha  Heche ni katibu wa chadema mkoa wa mara alisema kuwa baadhi ya viongozi wakiwemo madiwani wamekamatwa na kubambikiwa kesi ikiwa ni pamoja na kuwekewa pingamizi la kuchukua fomu za kugombea nyadhifa za uongozi.

“Diwani wangu wa Serengeti pamoja na watendaji wangu wamekatwa na kuwekwa ndani na wengine wanabambikiwa kesi za meno ya Tembo ili chama changu kiweze kuanguka” alisema Chacha.

Kwa upande wake saguda joseph Mnawa mwenyekiti wa chadema wilaya ya Serengeti ambaye pia ni mwenyekiti wa  ulinzi na usalama kanda ya ziwa anazidi kukemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa  serikali.

“Tunasema hatutaogopa hatutakejeri mtu bali tunachotaka ni haki kutendeka kwa wananchiwetu” aliseama.

Aliongeza kuwa  viongozi wa serikali ndio chanzo kikubwa cha uchochezi wa fujo pale wanapotafuta sababu zisikuwa za msingi ili kuweza kuwakamata viongozi wa chama pinzani waweze kupata nafasi ya kupenya waondokane na vitendo hivyo na kuachia wananchi waweze kufanya maamuzi yao.


                                                             ….Mwisho…..



No comments:

Post a Comment