Monday, November 3, 2014

Ondoeni koo pamoja na ukabira ili kujenga maabara


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime ambaye pia ni diwani wa kata ya Sirari Amos Sagara katikati akikabidhi mifuko 10 ya saruji kwa wananchi wa kijiji cha Nyamuunda kata ya Mwema kwa ajili ya kuongeza nguvu katika ujenzi wa mahabara




Wananchi wilayani Tarime mkoani mara wametakiwa kuondokana na suala la kuendekeza matabaka ya koo  na ukabira katika suala la kuleta maendeleo kwani baadhi ya wananchi wameweza kutumia koo ili kuleta ubaguzi katika suala zima la kuchangia fedha za ujenzi wa maabara kutokana na agizo la Rais wa jamhuri ya mhungano wa Tanzania Dr jakaya Murisho kikwete.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa kata ya Mwema wilayani hapa Petro Ntogoro Kurate kipindi akipokea msaada wa mifuko kumi ya saruji yenye thamani ya shilingi laki mbil na thelathini  kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambaye pia ni diwani wa kata ya Sirari Amos Sagara ikiwa ni moja ya kuunga mkono wananchi katika ujenzi unaoendelea wa maabara.
Diwani huyo alisema kuwa katika kata yake ambayo ni kata ya Mwema wananchi wamechelewesha ujenzi wa maabara kwa sababu ya kuwepo kwa mvutano wa koo na  koo pamoja na ubaguzi wa makabira huku wakitaka kati ya koo ya wanchali na walinchoka nani ajenge maabara suala ambalo limepelekea kucheleweshwa kwa ujenzi huo.
“Lakini kwa sasa wananchi tumeanza kuwaelimisha na kuondokana na tabaka za  koo na wameanza kutekeleza ujenzi hivyo kufikia wiki ijayo tutakuwa tumefikia sehemu kubwa”alisema diwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime ambaye pia ni diwani wa kata ya Sirari Amos Sagara katika kuunga nguvu ya wananchi ametoa mifuko 10 ya saruji katika shule ya Sekondari Mwema  iliyopo kijiji cha Nyamuunda  kata ya Mwema.
Aidha Sagara amezidi kuamasisha wananchi kuendelea na ushirikiano katika ujenzi wa maabara na kukemea baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao wameingilia zoezi la tamko la rais wa jamhuri ya Tanzania kuhusina na ujenzi wa maabara nasuala ambalo linapelekea  kugoma kwa wananchi na kurudisha maendeleo ya Taifa Nyuma
 “Wananchi msikubali kutumika vibaya na viongozi kiongozi akija muulize ameleta nini ili kuongeza nguvu ya ujenzi kama ni siasa tusubili 2015” alisema sagara.
Mwenyekit huyo aliongeza kuwa Halmashauri yake shule zenye uitaji wa maabara ni 24  na uitaji wa maabara ni 67 lakini shule ambazo zimeonesha mwamko mkubwa katika ujenzi  ni shule 4 ikiwemoshule yake ya Sirari Sekondari, Kibasuka, Inchugu na Nyamwigura Sekondari.
“ Sisi kama Serikali Tunaenda kuwapa  nguvu wale ambao wameonesha mwamko wa kujenga haraka   ili kuweza kumaliza zoezi  ” alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime.
Wananchi wa kijiji cha Nyamuunda kata ya Mwema walisema kuwa kwa sasa wameanza kutekeleza agizo la Rais ili watoto wao waweze kusoma kwa vitendo masomo ya sayansi.
“Kupitia kikao tulikubaliana kilia Mwananchi atachanga shilingi Elfu kumi lakinki kwa sasa hali ya uchumi ni mbaya hivyo tumeanza kuchanga Elfu tatu kwa awamu ili kufanikisha zoezi”walisema wananchi hao.
                       ……… Mwisho…

No comments:

Post a Comment