Friday, October 24, 2014

Mwanamke ashambuliwa kwa mshale katika makalio Tarime



Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Bunyige Chacha 25 mkazi wa kata ya mriba wilayani Tarime Mkoani Mara ameshambuliwa kwa mshale sehemu za makalio kwenye  mguu wake wa kulia suala ambalo limemsababishia maumivu makali.
Mwanamke huyo aliyeshambuliwa na mume wake aliyejulikana kwa jina la  Ghati Nyamarandi mkazi wa mriba wilayani Tarime  mkoani hapa  amesema kuwa mmewe alimshambulia baada ya kuulizwa watoto aliokuwa akiwapeleka na kuwaozesha badala ya kuwachisha shule na kuozeshwa nyumba Ntobhu.
Bi: Chacha alisema kuwa mmewe alipeleka binti wa kwanza ambaye alikuwa kidato cha tatukatika shule ya sekondari sirari na kuozeshwa nyumba Ntobhu huku wilayani mugumu na kurudi na kupeleka binti wa pili ambaye alikuwa kidato cha pili shule ya sekondari Nyamaraga na kuozeshwa kata ya Nyamaraga wilayani Tarime.
Aidha mama huyo amesema kuwa amekuwa akifanya hivyo kwa lengo la kupata mahari ya kulipia mke wake wa pili.
Hata hivyo mama huyo amesema kuwa serikali pamoja na mashirika hawana budi kuzidi kukemea vitendo hivyo kwa lengo la kutimiza ndoto za watoto wa kike.
Zabron Mrimi ni msaidizi wa kisheria katika kata ya sirariamesema kuwa mama huyo amefika ofisini kwake na kutoa taarifa ndipo ameweza kumpeleka katika kituo kidogo cha polisi kilichopo Sirari ili kuwza kupewa matibabu katika hospitali ya binafsi ya Alpha iliyopo mji mdogo wa Sirari.
Mama huyo kisa hicho kilimpata October 5 mwaka huu na ndipo aliweza kukimbilia kwa dada yake katika maeneo ya soko la Sirari wilani Tarime na jana aliamua kutoa siri hiyo na kupelekwa hosipitali kwa matibabu.
                           ….Mwisho…
 

No comments:

Post a Comment