Monday, November 10, 2014

MAHAKAMA YA MWANZO RYAGORO YACHOMWA MOTO.



MAHAKAMA ya Mwanzo Ryagoro Wilayani Rorya Mkoani Mara imechomwa Moto na watu wasiofahamika na kuteketeza chumba cha masijala pamona na vielelezo vya kumbukumbu za mafaili kuteketea.

Akisimulia tukio hilo kwa waandishi wa habari Kamanda Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya kamishina msaidizi wa Jeshi la polisi ACP Lazaro Mambosasa alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 3.30 usiku  kuamkia November 09  mwaka huu. 

''Jengo la Mahakama ya Mwanzo Ryagoro lilichomwa moto na watu wasiojulikana chumba kilichoathirika zaidi ni chumba cha masijala ya mahakama hiyo dhamani ya mali iliyoungulia ndani ikiwa ni majalada pamoja na samani nyingine ni Tsh 5,000,000''alisema Mambosasa.

Aidha Mambosasa aliongeza kuwa hakuna Mtu yeyote ambaye anashikiliwa kuhusiana nan tukio hilo na kuwa chanzo cha tukio bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea kufanya upelelezi kuwapata watuhumiwa wa tukio hilo na kuwafikisha kunako husika.

Kwa upande wa wananchi wa kutoka eneo la tukio walisema kuwa mahakama hiyo iliunguzwa saa 2 usiku kuamkia Novemba,9 mwaka huu na watu ambao wanasadikiwa kuwa ni watuhumiwa wa makosa mbalimbali.

''Vijana walikuwa wanatoka usiku katika majumba ya kuonyesha mpira gafula  walipita wakaona Jengo la mahakama linaungua moto ambapo walipiga mwana ili kuomba msaada ambapo wananchi walifika na kutoa msaada wa kuokoa mali zilizokuwemo ndani yake''walisema wananchi hao.

Aidha wananchi hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe Gazetini walisema kuwa kuchomwa moto mahakama hiyo ni kupoteza kumbukumbu za mafaili ya watuhumiwa ambao walikuwa wanashitakiwa mahakamani hapo.
 
''Tunaomba serikali ichukue hatua za haraka kuwasaka watuhumiwa wa tuykio hilo kwa sababu kitendo hiki hakifurahishi jamii na kina lengo la kudididmiza wanyonge''walisema wananchi hao.
                                           
                                                       ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,

Zaidi ya vijana 250 wamepata ajila kupitia uchimbaji mdogo.


Wachimbaji wadogo katika mgodi wa Musega kijiji cha Genkuru kata ya Nyarukoba wilayani Tarime 
Mkoani Mara  wakiponda mawe kwa ajili ya kuuzia wateja na badae kupembua na kupata  dhahab







Zaidi ya vijana 250 wakiwemo wakina mama, na wazee wamepata ajila katika mgodi wa wachimbaji wadogo wa Musega uliopo katika kijiji cha Genkuru kata Nyarukoba Wilayani Tarime Mkoani Mara suala ambalo limewasaidia kukidhi mahitaji yao huku baadhi ya vijana wakiondokana na uvamizi wa migodi pamoja na uwindaji haramu ambao walikuwa wakifanya hapo awali kabla ya kupata ajila hizokatika vijiji ambavyo ni jirani na hifadhi ya Mbuga ya wanyama 

Akiongea na Gazeti hili mmoja wa wamiliki wa Mgodi huo Ngicho Daud alisema kuwa ameweza kuajili vijana zaidi ya 250 wakiwemo wazee na akina mama.

“Kwa upande wa vijana tumewaajili kwa lengo la kupunguza uvamizi wa migodi pamoja na uwindaji haramu kwa sababu hapa wanafanya kazi masaa yote nakujipatia kipato kikubwa”alisema Ngicho.

Aliongeza kuwa  mgodi huo ulianzishwa na watu watatu lakini mpaka sasa watu wengi wameweza kujipatia ajila kupitia mgodi huo japo anakumbwa na changamoto kama vile ukosefu wa vifaa vya kisasa, ,Maeneo ya kutosha , Mtaji mkubwa kwa ajili ya kupanua Miradi ya uchimbaji huo.

 Sibute Masero ni mmoja wa vija ambao wamepata ajilia kupitia mgodi huo wa wachimbaji wadogo alisema kuwa ameamua kuacha suala la uwindaji haramu na kujiingiza katika uchimbaji mdogo kwa lengo la kupata kipato cha harari.
“Katika uwindaji haramu niliweza kufungwa kilia gereza lakini nilifanikiwa kutoka hivyo  inabidi niendelee na kazi yangu ya uchimbaji mdogo ili kupata kipato changu” alisema Sibute.

Kwa upande wake Pusinya Kichugu mkazi wa Kijiji cha Genkuru alisema kuwa kutokana na kununua mawe hayo ameweza kusomesha watoto wawili sekondari na kukidhi mahitaji yake yote ya Nyumbani.
                        
Wakina mama tuliowengi tunategemea Machimbo haya madogo kikubwa tunaomba serikali iltuletee  vifaa vya kisasa ili tuweze kuboresha uchimbaji wetu alisema Pusinya
                             

                                                   ….MWISHO…

Sunday, November 9, 2014

Vijana watakiwa kulinda nguvu ya Taifa



Naibu mwenyekiti wa baraza la wanawake BAWACHA Hawa mwaifunga akiongea na wananchi kwenye mkutano wa adhara kuhusu rasimu ya katiba

Vijana wametakiwa kulinda nguvu ya Taifa ikiwa ni pamoja na kufanya mapinduzi na maamuzi ya kweli ili kuweza kupata viongozi na si kuchagua viongozi mizigo ambao watachosha wananchi na kufuja mali za umma 

Kauli hiyo Mratibu wa uhamasishaji wa vijana Chadema Taifa Edward Simbey  katika mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni katika mji mdogo wa Utegi  wilayani Rorya Mkoani Mara katika mwendelezo wa ziara ya kuelimisha wananchi kuhusu chaguzi za serikali za mitaa pamoja na maoni juu rasmu ya katiba mpya  huku wakiambatana na viogozi wa kitaifa Balaza la akina Mamakupitia Chama Cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA chini ya Mwenyekiti akina Mama Bawacha Taifa Halima Mdee.

 Edward alisema kuwa taifa lolote duniani vijana ndo nguvu kazi ya taifa katika chachu ya kusukuma gurudumu la Maendeleo ikiwemo na wilaya ya Rorya.

Aidha  Mratibu wa vijana aliwataka vijana hao Vijana waoneshe nguvu ya jeshi ili kuwepo upambanaji wa kweli mpaka haki inapatikana huku akilaani jeshila polisi kuondokana na kunyanyasa vijana na kuwageuza mitaji na kuwatengenezea kesi zisizokuwa za msingi ili kuweza kujipatia maslahi.

Kwa upande wakeMbunge wa Viti maalumu Ester Matiko ambaye pia ni Mwenyekiti akina Mama Mkoa wa Mara  alisema kuwa akina mama hospitalini wamezidi kuangaika na kununua madawa wakati serikali inazidi kutumia fedha kubwa katika mambo yasiyo ya msingi.

“Wanafunzi sasa wanatahabika kwa kukosa  Madawati, Madarasa yanadodondoka kwanini nhizo fedha serikali inazoharibu zisije kujenga shule na kununua madawati” alisema.

 Naye katibu wa Mkoa mkoa wa Mara Chacha Heche amezidi kulaani viongozi wanaotumia ubabe kunyanyasa wananchi kuondoka na  vitendo hivyo mara moja.

Hata hivyo meya wa manispaa ya musoma Alex Kisurula  alisema kuwa alisema kuwa maendeleo yanletwa na viongozi wenye uzalendo pamoja na siyo viongozi wanaojitapa kwa utajili walionao wakati wananchi wanazidi kutaabika.

Maisha yangu yanfanana na wananchi wa ngu lakini nyie wananchi wa Rorya maisha mbunge wenu yanafanana na ya kwenu alisema meya.

Pia meya huyo aliwataka wananchi wa rorya kuondokana na vijazawadi wanavyopatiwa  na kubadilisha mawazo katika kupiga kura na kuchagua viongozi wabovu. 
                                                 ....mwisho.........

MAKUMBUSHO YA BABA WA TAIFA YATUNZWE..



Serikali imetakiwa kutunza makumbusho ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambalage Nyerere ili yaendelee kuwepo kwa lengo la kizazi kijacho.

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu katibu mkuu Balaza la wanawake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kunti Yusuph kwenye ziara ya kutembelea makumbusho uya Baba wa Taifa katika kijiji cha Mwitongo wilayani Butiama.

Naibu hiyo alisema kuwa serikali nimekuwa ikitumia fedha nyingi lakini imesahau kutunza makumbusho ya baba wa taifa katika hadhi ya kimataifa 

“Tumetembelea makumbusho ya Baba wetu wa taifa lakini huwezi kuyathaminisha na  yale alikuwa akiyafanya hayati Julius Kambalage” aalisema Naibu.

Naye mbunge wa viti maalumu jimbo la Tarime Mkoania Mara Ester Matiko amezidi kulaani vitendo vya vifo kwa akina mama nakuwataka kuungana pamoja ili kutokomeza vifo hivyo.

“Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni Mwanamke lakini tunaendelea  kufaliki tunaomba jeshi la polisi kujipanga sawa na si kuja kurekodi mikutano ya Chadema na kushindwa kusaka waoua” alisema Matiko.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu Grace kiwelu aliwataka wananchi kuondokana na ukabira,pamoja na  udini ili kudumisha Amani, Upendo na Mshikamano.

Katika uhai wa hayati Nyerere alipinga sana ukabira iweje kwa sasa chama cha CCM kishindwe kutetea yale aliyoyaacha Baba wa Taifa.

Hata Mmoja wa kutunza makumbusho hayoBaraka Bwire katika kutoa historia ya Hayati lasema kuwa wanakabiliwa na ukosefu wa fedha ili kuendeleza makumbusho hayo.

“Ruzuku zinatengwa kutoka serikalini lakini zinafika zikiwa zimechelewa na wakati mwingine ufika kidogo na kusababisha ukosefu wa fedha zaq kuendeshea na kuboresha  makumbusho haya” alisema Bwire.

                                                 ……MWISHO…

Thursday, November 6, 2014

WAOMBOLEZAJI WASHUSHIWA KIPIGO NA POLISI- TARIME


Katika hali isiyokuwa  ya kawaida waombolezaji wa mazishi ya kijana John msonso Christopher wa kijiji cha Kewanja wilayabi Tarime  mkoani Mara alie uawa kwa kuvunjwa shingo na watu wasio julikana, wamepata kipigo kutoka kwa askari  polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya na kusababisha watu watatu kulazwa katika kituo cha afya cha nyangoto wilayani humo  


 Bw Mahanga buruna nahanga mkazi wa kijiji cha kewancha kitongoji cha magena ni mmoja kati ya watu walio jeruhiwa.

Kutoka na tukio hilo katibu wa ccm wa wilaya ya Tarime Bw Bogomba Rashidi na mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha kewanja  Bw Tanzania Omtima ambao ni baadhi ya mashuhuda na ni  kati ya waombolezaji walio nusurika kupata kipigo kutoka kwa askari hao wamewataka vijana hasa wanao ishi kata ya matongo na kemambao kutii sharia bila shuruti ili kupunguza migogoro inayo jitokeza mara kwa mara baina ya polisi na vijana wa  kata hizo

 migogoro hiyo inasababisha baadhi ya vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kupoteza maisha uku takwimu zikionyesha kwamba kila mwezi vijana watatu mpaka watano wa vijiji vinavyo zunguka mgodi huo hupoteza maisha na kuacha wajane na watoto yatima  ambao badae watakuwa mzigo mkubwa kwa serikali katika kuwatunza

Pia viongozi hao wamelitaka jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya nalo lisitumie nguvu nyingi kupita kiasi katika kupambana na wananchi wa kata hizo na badara yake wawakamate watuhumiwa na kuwafikisha katika vyombo vya sharia  

                                                        Mwisho

Wednesday, November 5, 2014

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime azidi kuungamkono wananchi katika ujenzi wa maabara.






Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambaye pia ni diwani wa kata ya Sirari amezidi kuonesha moyo wa kuchangia ujenzi wa maabara unaoendelea katika shule za sekondari wilayani Tarime ili kuweza kuwaunga mkono wananchi.

Mwenyekiti huyo ikiwa ni moja ya kukagua miradi ya ujenzi wa maabara hizo ameweza kutoa msaada wa mifuko 13 ya saruji katika shule ya sekondari Kibasuka ambapo hivi karibuni ameweza kutoa mifuko 10 ya sarujiu katika shule ya sekondari Mwema kwa lengo la kuwaunga  mkono wananchi hao.

Sagara alisema kuwa suala la ujenzi wa maabara ni la kila mtu hivyo wananchi hao hawana budi kuzidi kuonesha mshikamano, Umoja na Nguvu ili kuweza kukamilisha ujenzi huo.

“Sisi kama serikali wale ambao wataonesha moyo wa kujenga tutawapa kipaumbele pale tutakapo anza kusambaza fedha za kusaidia kusukuma ujenzi huo” alisema sagara.
Kwa upande wake Mtendaji wa kata ya Kibasuka Mwita Marwa Mtatiro alisema kuwa yeye ameweza kutumia njia ya kuamasisha kupitia rika(Saiga) suala ambalo limeweza kusaidia katika kusukuma ujenzi huo kwa kiasi kikubwa sana.

“Jengo moja tayari limefikia katika renta hii yote ni nguvu ya wananchi na hapa wamekusanyika wanazidi kujadili na kurejesha michango”alisema Mtendaji.

Naye Diwani wa kata hiyo Joseph Moya Suleiman alizidi kuwataka wadau wote wa maendeleo wakiwemo wafanyabihashara kuzidi kujitolea kwa lengo la  kufanikisha

“Maabara ni kwa ajili ya watoto wetu endapo tutamaliza ujenzi huu tutazalisha wanasayansi wengi kutokana na shule zetu za kata” alisema Moya.

                                              …..MWISHO…